Wanafunzi wanne kizimbani kwa kumkashifu Rais
Wanafunzi wanne kizimbani kwa kumkashifu Rais
Wanafunzi
wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala Dar es Salaam, wamefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakikabiliwa na shitaka la kuchapisha picha
zinazoonyesha Rais Dk. John Magufuli amevaa hijabu kama mwanamke wa
Kislamu na kuzisambaza kwenye mtandao wa WhatsApp.
Shtaka jingine ni kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya amii (WhatsApp) kwa lengo la kumuudhi Rais.
Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo (19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel (21) na Anne Mwansasu(21).
Walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Catherine Kiyoja.
Akisoma
mashitaka hayo, Wakili wa Serikali, Florida Wenceslaus, alidai
washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 9, mwaka jana Dar es Salaam.
Florida
alidai washitakiwa kwa pamoja walitengeneza picha hizo kwa kutumia
kompyuta na baadaye kuisambaza kwenye WhatsApp kwa lengo la kumuudhi
Rais.
Washitakiwa
walikana shitaka hilo na kurudishwa rumande kutokana na kutotimiza
masharti ya dhamana. Kesi itatajwa tena Machi 13, mwaka huu.
No comments: