Masogange apandishwa kizimbani, aachiwa kwa Dhamana ya Milioni 10
Msanii
Agnes Gerald 'Masogange' amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka ya kutumia dawa za kulevya.
Mrembo
huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo
fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 2i mwaka
huu.
Katika
mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri
Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa
kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan kwa nyakati tofauti.
Mara baada ya kusomewa mashtaka yake, ameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.
Pia
mrembo huyo ambaye amewahi kukamatwa nchini Afrika Kusini akihusishwa
na usafirishaji wa dawa za kulevya, ametakiwa kutotoka nje ya Dar es
Salaam kwa kipindi chote cha kesi bila kibali cha mahakama.
No comments: