Zitto Kabwe azidi kuibana Serikali Kuhusu ufisadi wa IPTL....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua
Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea
kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita ufisadi katika
kampuni ya uzalishaji umeme ya IPTL, inayomilikiwa na Kampuni wa PAP.
Tangu
Rais Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2015, Zitto
amekuwa mstari wa mbele kumsihi na kumuomba Rais Magufuli afanye maamuzi
juu ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikilipwa milioni 300 kila siku bila
kujali kama inazalisha umeme au la.
Kupitia
mitandao ya kijamii, Zitto ameandika "Rais John Magufuli ana fursa ya
kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka
mwaka 1995. watanzania masikini na wanyonge tutakuwa nyuma yake kwenye
hili. Atende sasa."
Mnamo
tarehe 21, Septemba 2016 Mhe. Zitto Kabwe alimtaka tena Rais Magufuli
aoneshe hasira zake dhidi ya hicho anachokiita ufisadi mkongwe wa IPTL
huku akieleza masikitiko yake juu ya kutochukuliwa kwa hatua zozote hadi
sasa.
Mhe.
Zitto Kabwe ambaye amekuwa hachoki kulizungumzia sakata hilo la IPTL
amehoji ni nini kipo nyuma ya pazia, na ni nani mfaidika hadi hatua
zisichukuliwe, huku akitoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na
mahakama kwa sasa.
"Mahakama
Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa.
Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota
mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m
kila siku izalishe au isizalishe umeme? Ushahidi wote ulionyesha utapeli
wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha
uamuzi wa Mahakama umefanya matapeli hawa kuendelea kunyonya fedha
kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc?
Ama ni jipu la mgongoni?". Alihoji Mhe. Zitto Kabwe
No comments: